Top Ad unit 728 × 90

Mchezo Wa Mashabiki Wa Simba Na Yanga Nani Mtani Jembe Simba Wangara Chuo Cha AJTC.

KIKOSI CHA SIMBA {AJTC} 
Mechi ya nani mtani jembe kati ya mashabiki wa timu ya Simba na Yanga wa chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Arusha imekamilika baada ya timu ya Simba kuibuka na ushindi wa bao 2-1.
Mechi hiyo imechezwa katika viwanja vya Field Force kwa morombo jijini Arusha.
Timu ya Simba iling'ara mara baada ya mchezaji Salum Langa kufunga bao la kwanza mnamo dk ya 21 na kuwainua mashabiki wa Simba kwa vifijo.
KIKOSI CHA YANGA WALIO VALIA BLU {AJTC}
Hadi mapumziko Simba walikuwa wanaongoza kwa bao 1 huku Yanga wakiwa hawajapata kitu.
Simba iliendeleza wimbi la ushindi mara baada ya mchezaji wake Saleh Abdalah kucheka na nyavu mnamo dk ya 75 na kiandikia timu yake bao la 2.
Yanga walipata bao lao la kufutia machozi kupitia kwa mchezaji Gilbert  Johansen mnamo dk ya 84 baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa mchezaji Aziz Mwinuka.

Baada ya mechi kukamilika mashabiki wa timu zote mbili walikuwa wakijitamba huku wachezaji wa Yanga wakisema kesho ndio watajua nani zaidi katika mechi ya kweli kati ya Simba na Yanga.
JIMMCARTER.COM WANAKUTAKIA HERI YA SIKUKU NA MAANDALIZI MEMA YA SIKUKU YA CHRISTMAS NA MWAKA MPYA PIA TUNAKUKRIBISHA KUJIUNGA NASI HAPA CHINI 
HABARI NA JIMMY MINJA
Mchezo Wa Mashabiki Wa Simba Na Yanga Nani Mtani Jembe Simba Wangara Chuo Cha AJTC. Reviewed by Unknown on 10:26 AM Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by Pamoja We Can © 2014 - 2015
Designed by Sweetheme Team | Share by HowLoad

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.